Comunidad Autonoma de Canarias Jimbo la Kujitawala la Visiwa vya Kanari | |
Miji Mikuu | Santa Cruz de Tenerife Las Palmas de Gran Canaria |
Eneo
|
|
Wakazi
|
|
Uwakilishi bungeni
|
14 |
Rais wa serikali ya Kanari | Adán Martín Menis (CC) |
Tovuti rasmi | Gobierno de Canarias |
Visiwa vya Kanari (kwa Kihispania: Islas Canarias) ni funguvisiwa la Afrika ya Kaskazini katika bahari ya Atlantiki. Viko baharini km 150 magharibi kwa Moroko. Umbali na Hispania ni masaa mawili kwa ndege.
Visiwa vikubwa ni saba:
El Hierro, La Gomera, La Palma na Tenerife ambavyo vinaunda mkoa wa Santa Cruz de Tenerife,
halafu Gran Canaria, Fuerteventura na Lanzarote ambavyo vinaunda mkoa wa Las Palmas,
tena kuna visiwa vidogo sita vya Alegranza, Kisiwa cha Lobos, La Graciosa, Montaña Clara, Roque del Este na Roque del Oeste, vyote vya mkoa wa Las Palmas.