Vita vya Kagera (kwa Kiingereza: kwa Kiingereza: Uganda-Tanzania War) ni vita vilivyopigwa kati ya Uganda na Tanzania kuanzia tarehe 30 Oktoba 1978 hadi 11 Aprili 1979.
Vita hivyo vilihusu kugombania ardhi ya mkoa wa Kagera kati ya nchi ya Tanzania na Uganda.
Katika vita hivyo Tanzania, ikiongozwa na rais Julius Nyerere iliibuka kidedea kwa kuwapiga vema majeshi ya gaidi Idd Amini Dadah yaliyoungwa mkono wa Libya ya Muammar al-Gaddafi na pia Palestina ya Yasser Arafat.
Vita hivyo viliua watu karibu 5,000 na wengine kuachwa yatima.