Wamisionari wa Upendo ni shirika la kitawa la Kanisa Katoliki lililoanzishwa na Mama Teresa huko Kolkata, India mwaka 1950[1], ili kusaidia watu walio fukara zaidi duniani kote[2] .
Kufikia mwaka 2020 masista wake, wakiwemo waliojifungia kusali tu na wanaohudumia watu pia, walikuwa 5,167 katika nchi 139.