Wangoni ni kabila la watu wa Kusini mwa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Ruvuma, hasa upande wa kusini wa Songea. Pia kihistoria yapo makundi yaliyoingia upande wa magharibi mwa Tanzania. Pia wako Msumbiji.
Asili yao ni Wazuluwalioenea kutoka Afrika Kusini, sehemu inayofahamika kama KwaZulu-Natal, kufuatia mapigano kati ya Makaburu na Wazulu yaliyotokwa katika karne ya 19.
Pengine Wangoni wamelaumiwa kwa kujificha kuonesha maarifa yao hasa katika sanaa ya muziki na maigizo. Pia katika masuala ya elimu na biashara wao si washiriki wakubwa, mwamko ni mdogo. Ikumbukwe kuwa Wangoni waliowahi kuvuma katika muziki na maigizo ambao wamekulia Songea ni Bambo na kapteni Komba. Lakini inaonekana kuwa Wangoni ni maarufu sana katika kuimba katika sherehe na maombolezo; wana nyimbo nyingi kwa ajili hizo. Pia katika sanaa ya muziki hupenda kujitokeza kama kundi: fuatilia ngoma zao kama Mganda na Kihoda, Lizombe, Beta n.k.
Wangoni wamekuwa wakipoteza uhalisia wao kwa sababu ya kulowea: wanakoenda kukaa hujichanganya mapema na tamaduni za makabila mbalimbali mahalia. Kwa mfano leo kuna Wangoni Wamatengo, Wangoni Wanyasa, Wangoni Wampoto... Jambo hilo ni matokeo ya Wangoni kutopenda kuonesha asili yao, Mfano lugha... ni kama kusema Wangoni ni kabila lilioelewa sana somo la kutojali ukabila. Leo hii tunaweza kuwatambua Wangoni kwa majina yao tu ambayo mengi ni ya wanyama au viumbe hai kama Komba, Mbawala, Mapunda, Tembo, Nguruwe, Simba, n.k. na katika matukio ya kijamii lakini sio katika uhalisia wa maisha ya kila siku.
Pia kuna kujitazama zaidi na kuona kuwa mambo ya muziki na sanaa, biashara na uchumi na elimu si ya hadhi yao, yaani kuna ile hali ya kujiona mkubwa kuliko jambo fulani, yaani Mngoni kuuza ndizi ni kujidhalilisha au kucheza muziki ni jambo ambalo si la heshima na linalokubalika katika jamii. Mfano ni katika kipindi cha miaka ya karibuni kumekuwa na wanawake wanaofanya biashara ndogondogo, asilimia kubwa wanaamini katika kilimo.
Vilevile, kutokana na sifa ya ukubwa wa kabila la Wangoni, basi makabila yanayolizunguka nao wanajiita Wangoni. Hivyo kuna hatari ya baadhi ya makabila madogomadogo kupoteza utambulisho wao.