Wilaya ya Korogwe ni mojawapo kati ya wilaya 11 za Mkoa wa Tanga katika pwani ya Tanzania.
Mwaka 2002 ilikuwa na wakazi 261,004 [1]. Mnamo 2011 Wilaya ya Korogwe Mjini ilitengwa. Mwaka 2012 waliobaki upande wa vijijini walikuwa 242,038 walioishi katika kata 20 za wilaya. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 272,870 [2] katika tarafa 4, kata 29 na vijiji 118..
Makao makuu ya wilaya yako Korogwe mjini.
Kuna shule za msingi 118 na sekondari 27 na vituo vya afya 3.
Misimbo ya posta ya wilaya hii huanza kwa tarakimu 216[3].