Wilaya ya Masasi ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Mtwara. Maeneo ya mji wa Masasi yalikuwa sehemu ya wilaya hii lakini tangu mwaka 2011 mji ulipata halmashauri yake kwa hiyo kama wilaya ya pekee.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 247,993 [1]
Masasi ni wilaya kubwa ya Mtwara; inapakana na Mkoa wa Lindi upande wa kaskazini, Mkoa wa Ruvuma upande wa magharibi na nchi ya Msumbiji upande wa kusini. Upande wa mashariki kuna mpaka na wilaya ya Newala.
Eneo la wilaya ni 4,429 km² linajumlisha asilimia 23 ya eneo lote la Mkoa wa Mtwara.
Kuna majimbo ya uchaguzi wa bunge mawili ambayo ni Lulindi na Masasi.
Vitengo vya chini ni tarafa 5, kata 22, vijiji 170 na vitongoji 986.[2].