Wilaya ya Meru ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Arusha yenye postikodi namba 23300.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Meru ilihesabiwa kuwa 268,144 [1]. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 331,603 [2].
Wilaya hiyo ilianzishwa kutoka maeneo ya wilaya ya zamani ya Arumeru iliyogawiwa kuwa wilaya ya Arusha Vijijini na wilaya ya Meru.
Makao makuu ya wilaya yako mjini Usa River.