Wilaya ya Nyasa

Malori yanakwama njiani kwenda Mbamba Bay wakati wa mvua (mwaka 2012).

Wilaya ya Nyasa ni wilaya mojawapo kati ya 8 za Mkoa wa Ruvuma, yenye postikodi namba 57500, ambayo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 kutokana na maeneo ya wilaya ya Mbinga. Eneo la wilaya hii liko kando ya Ziwa Nyasa.

Makao makuu ya wilaya yako Mbamba Bay.

Wakati wa sensa ya mwaka 2012, wilaya ilikuwa na wakazi 146,160. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 191,193 [1].

  1. https://www.nbs.go.tz

Wilaya ya Nyasa

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne