Wilaya ya Rorya

Rorya ni wilaya mojawapo kati ya 9 za mkoa wa Mara yenye postikodi namba 31300. Hadi mwaka 2006 ilikuwa sehemu ya magharibi ya wilaya ya Tarime.

Makao makuu ya Wilaya ya Rorya ni Ingri Juu (31311 Mirare).

Eneo la wilaya liko kati ya ziwa Viktoria Nyanza upande wa magharibi na Tarime upande wa mashariki. Upande wa kaskazini inapakana na nchi ya Kenya na upande wa kusini na wilaya ya Musoma.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, wilaya hii ilikuwa na wakazi wapatao 265,241 waishio humo [1] na katika ile ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 354,490 [2].

Walio wengi ni Waluo. Makabila mengine ni Wakine, Wakurya, Wasimbiti, Wahacha, Wasweta na mengineyo. Hii ndiyo wilaya yenye makabila mengi zaidi nchini Tanzania.

  1. Sensa ya 2012, Mara - Rorya-District-Council
  2. https://www.nbs.go.tz

Wilaya ya Rorya

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne