Wilaya ya Serengeti ni wilaya mojawapo kati ya 9 za Mkoa wa Mara yenye postikodi namba 31600.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 249,420 [1] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 340,349 [2].
Sehemu kubwa ya wilaya ni eneo la hifadhi ya Serengeti iliyo mashuhuri kote duniani.
Makao makuu ya wilaya yapo Mugumu mjini.