Tarime Wilaya ya Tarime |
|
Mahali pa Wilaya ya Tarime | |
Mahali pa Wilaya ya Tarime |
|
Majiranukta: 1°24′51″S 34°27′51″E / 1.4141°S 34.4642°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mkoa wa Mara |
Wilaya | Tarime |
Eneo | |
- Jumla | 1,371 km² |
Idadi ya wakazi (Sensa ya 2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 404,848 |
EAT | (UTC+3) |
Tovuti: https://tarimedc.go.tz |
Wilaya ya Tarime ni wilaya mojawapo kati ya 9 za Mkoa wa Mara. Zamani ilijulikana kwa jina la "Wilaya ya Mara Kaskazini". Mwaka 2006 sehemu ya mashariki ya Tarime imekuwa wilaya mpya ya Rorya.
Tarime imepakana na Kenya (kaunti za Migori, Trans Mara na Kisii) upande wa kaskazini na mashariki. Hifadhi ya wanyama ya Masai Mara ya Kenya uko upande wa mashariki pia. Upande wa kusini umepakana na wilaya za Musoma mjini, Musoma vijijini na wilaya ya Serengeti. Upande wa magharibi iko wilaya mpya ya Rorya.
Makao makuu ya wilaya yapo mjini Tarime.
Misimbo ya posta katika wilaya hii inaanza kwa 314.