William Ruto | |
William Ruto, 2022 | |
Aliingia ofisini 13 Septemba 2022 | |
Deputy | Rigathi Gachagua (2022–2024) Kithure Kindiki (2024–) |
---|---|
mtangulizi | Uhuru Kenyatta |
Muda wa Utawala 9 Aprili 2013 – 13 Septemba 2022 | |
Rais | Uhuru Kenyatta |
mtangulizi | Kalonzo Musyoka |
aliyemfuata | Rigathi Gachagua |
Waziri wa Elimu ya Juu
| |
Muda wa Utawala 21 Aprili 2010 – 19 Oktoba 2010 | |
Rais | Mwai Kibaki |
Waziri Mkuu | Raila Odinga |
mtangulizi | Sally Kosgei |
aliyemfuata | Hellen Jepkemoi Sambili (kaimu) |
Waziri wa Kilimo
| |
Muda wa Utawala 17 Aprili 2008 – 21 Aprili 2010 | |
Rais | Mwai Kibaki |
Waziri Mkuu | Raila Odinga |
mtangulizi | Kipruto Arap Kirwa |
aliyemfuata | Sally Kosgei |
Waziri wa Mambo ya Ndani
| |
Muda wa Utawala 30 Agosti 2002 – Desemba 2002 | |
Rais | Daniel arap Moi |
mtangulizi | George Saitoti |
aliyemfuata | Moody Awori |
Muda wa Utawala 29 Desemba 1997 – 9 Aprili 2013 | |
mtangulizi | Reuben Chesire |
aliyemfuata | (mbunge wa mwisho) |
tarehe ya kuzaliwa | 21 Januari 1967 Kamagut, Kenya |
chama | UDA (2021–) |
chamakingine |
|
ndoa | Rachel Chebet (m. 1991–present) |
watoto | 7, ikijumuisha Charlene |
makazi | Ikulu |
signature |
William Kipchirchir Samoei arap Ruto (alizaliwa Kamagut, wilaya ya Uasin Gishu, 21 Disemba 1966) ni mwanasiasa wa Kenya ambaye amekuwa rais wa tano wa nchi kuanzia tarehe 13 Septemba 2022.
Alikuwa Waziri wa Kilimo tangu Aprili 2008 akawa makamu wa rais tangu mwaka 2013 hadi 2022.
Ruto aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Kenya African National Union, chama cha siasa kilichotawala zamani. Pia, alikuwa mbunge wa Eldoret Kaskazini tangu mwaka wa 1997, akawa Waziri wa Mambo ya Ndani mnamo Agosti 2002 lakini alipoteza nafasi hiyo baada ya uchaguzi wa Desemba 2002, ambapo KANU ilipoteza kwa muungano wa NARC.
Baada ya uchaguzi wa Kenya ya tarehe 9 Agosti 2022 Ruto alitangazwa kuwa mshindi tarehe 15 Agosti 2022. Matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na mipaka nchini Kenya Wafula Chebukati yalikanushwa na makamishna 4 wa Tume Huru ya Uchaguzi. Mpinzani wake Raila Amolo Odinga alikataa matokeo hayo na kuwasilisha kesi kwenye mahakama ya juu ya Kenya. Hata hivyo uamuzi ulithibitisha uhalali wa matokeo yaliyotangazwa awali.