Yako ni mji wa Burkina Faso ya kaskazini na makao makuu ya wilaya ya Passore, katika mkoa wa Nord. Pamoja na vijiji katika eneo lake kuna takriban wakazi 77,000[1].
Iko kilomita 100 kaskazini-magharibi kwa Ouagadougou.
Kihistoria ilijulikana kama mji mkuu wa dola dogo na msikiti mkubwa.
Yako ni mahali ambako rais wa tano wa Burkina Faso Thomas Sankara alizaliwa na kuzikwa.