Zama za Chuma katika historia kilikuwa kipindi kirefu baada ya watu kuanza kutumia vifaa vya chuma. Kabla yake, walikuwa wakitumia vifaa vya shaba na awali mawe yaliyochongwa tu.
Sehemu nyingi za Ulaya, Afrika na Asia walifikia Zama hizi za Chuma kunako mwaka wa 500 KK. Kwa upande wa Ulaya, ni kipindi cha kabla ya historia, kwa sababu watu wa Zama za Chuma hawakuwa wakiandika kumbukumbu zao.