Zeituni au zaituni ni matunda ya mti mfupi wa familia ya Oleaceae (jina la kisayansi kwa Kilatini Olea europaea, yaani "mzeituni wa Ulaya", au Olea sylvestris, yaani "mzeituni wa msitu") unaopatikana hasa kandokando ya Bahari ya Kati, lakini pia sehemu nyingine za Afrika na Asia.[1]
Matunda yake ni muhimu hasa kwa utengenezaji wa mafuta (90%), ingawa yanaliwa pia bila kushindiliwa (10%).
Toka zamani mafuta hayo yalitazamwa kuwa bora yakatumika katika ibada mbalimbali.