Zumari (kutoka jina la Kiarabu; kwa Kiingereza "flute") ni ala ya muziki inayopigwa kwa kupulizwa mdomoni.
Umbo lake ni kama bomba jembamba upande wa mdomoni na pana upande unaotokea sauti.
Inapatikana kote duniani. Hewa inapulizwa ndani kwa mdomo kupitia shimo; mkondo wa hewa unapita kwenye kona kali ambako unaanza kutingatinga ukisababisha nguzo ya hewa iliyopo ndani ya bomba kutingatinga pia; mitetemo hii ni sauti.
Urefu wa bomba unafanya tabia ya sauti; kama ni fupi linatoa sauti ya juu; kama ni refu lina sauti ya chini.
Zumari nyingi huwa na mashimo kanda yanayofunikwa na kufunguliwa kwa vidole. Kwa kufungua shimo mchezaji anafupisha au kurefusha nguzo ya hewa ndani ya zumari inayotingatinga na kubadilisha sauti hivyo.
Kuna muundo kadhaa: