Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Agaro

Agaro (au Haggaro) ni mji ambao unapatikana kusini mwa Ethiopia, jimbo la Oromia.

Barabara ambayo hapo awali iliunganisha Agaro na Jimma "ilijulikana zaidi kwa kina kuliko urefu wake" hadi maboresho yalipo kamilika mnamo mwaka 1962. Barabara ya Bedele, yenye urefu wa kilomita 96, ilikamilishwa mnamo 1968 kwa gharama ya dola milioni 12 (Ethiopia) ,na kampuni ya Ufaransa Razel Frères. Agaro ni moja ya vituo muhimu zaidi vya biashara ya kahawa nchini Ethiopia. Taasisi ya Jimma ya Afya ya Umma (sehemu ya Chuo Kikuu cha Jimma) ni kituo cha kufundishia huduma za afya huko Agaro.

Agaro ulikuwa ni mji mkuu wa Ufalme wa zamani wa Gomma,Gomma iliposhindwa na Dejazmach Besha Abuye mnamo mwaka 1886.Kufikia 1958,mji huu yalikuwa moja ya maeneo 27 nchini Ethiopia yaliyowekwa kama Jiji la daraja la kwanza.Fitawrari Gebre Kristos, alianzisha mashamba ya kahawa miaka ya 1950 kwenye ardhi aliyorithi kutoka kwa babu yake Fitawrari Wossen. Baada ya mapinduzi ya Ethiopia, Gebre Kristos aliacha shamba lake na kustaafu; shamba lake lilitaifishwa na Tangazo la Utaifishaji Ardhi la Machi 1975.mji huu una shule za sekondari na za msingi,pia una shule kongwe za sekondari na za msingi.


Previous Page Next Page






አጋሮ AM Āgaro (lungsod) CEB Agaro English آگارو FA Agaro French Agaro Polish Агаро Russian Agaro Swedish 阿加羅 Chinese Agaro ZU

Responsive image

Responsive image