Kibukitan ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia na Malaysia inayozungumzwa na Wabukitan kwenye kisiwa cha Kalimantan. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kibukitan imehesabiwa kuwa watu 570 nchini Indonesia na 290 nchini Malaysia. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibukitan iko katika kundi la Kiborneo-Kaskazini.