Kicol (pia Kilembak au Kisindang) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wacol kwenye kisiwa cha Sumatra. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kicol imehesabiwa kuwa watu 145,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kicol iko katika kundi la Kimalayiki.