Kiijo-Mashariki (pia Kinembe) ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Wanembe na Waakassa. Mwaka wa 1977 idadi ya wasemaji wa Kiijo-Mashariki imehesabiwa kuwa watu 71,500. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiijo-Mashariki iko katika kundi la Kiijoidi.