Kikaurna kilikuwa lugha ya Kipama-Nyungan nchini Australia iliyozungumzwa na Wakaurna katika jimbo la Australia Kusini. Hakuna wasemaji ambao wamebaki kuongea lugha hii, yaani lugha ya Kikaurna ilitoweka. Hata hivyo, kuna watu ambao wameanza kujufunza lugha ya Kikaurna tena kwa ajili ya kuihuisha. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikaurna kiko katika kundi la Kiyura.