Kikirike ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Wakirike. Mwaka wa 1995 idadi ya wasemaji wa Kikirike imehesabiwa kuwa watu 248,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikirike iko katika kundi la Kiijoidi. Wataalamu wengine wanaiangalia kama lahaja ya Kikalabari.