Kikubu (pia Kianak-Dalam) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wakubu kwenye kisiwa cha Sumatra. Mwaka wa 1989 idadi ya wasemaji wa Kikubu imehesabiwa kuwa watu 10,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikubu iko katika kundi la Kimalayiki.