Kilamaholot (pia Kisolor) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Walamaholot kwenye kisiwa cha Flores, Alor, Solor na vinginevyo vya jirani. Mwaka wa 2010 idadi ya wasemaji wa Kilamaholot imehesabiwa kuwa watu 180,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kilamaholot iko katika kundi la Kibima-Lembata.