Kinjebi ni lugha ya Kibantu nchini Gabon na Jamhuri ya Kongo inayozungumzwa na Wanjebi. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kinjebi nchini Gabon imehesabiwa kuwa watu 120,000. Pia kuna wasemaji zaidi ya 15,000 nchini Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinjebi iko katika kundi la B50.