Kinsenga ni lugha ya Kibantu nchini Zambia inayozungumzwa na Wansenga. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kinsenga nchini Zambia imehesabiwa kuwa watu 544,000. Pia kuna wasemaji nchini Msumbiji na Zimbabwe. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinsenga iko katika kundi la N40.