Kipatani ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wapatani kwenye kisiwa cha Halmahera. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kipatani imehesabiwa kuwa watu 10,600. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipatani iko katika kundi la Kihalmahera-Kusini.