Alaska | |||
| |||
Nchi | Marekani | ||
---|---|---|---|
Mji mkuu | Juneau | ||
Eneo | |||
- Jumla | 1,717,854 km² | ||
- Kavu | 1,481,347 km² | ||
- Maji | 236,507 km² | ||
Tovuti: http://www.alaska.gov/ |
Alaska ni kati ya majimbo ya kujitawala ya Marekani. Iko kaskazini kabisa kwenye bara la Amerika ya Kaskazini. Alaska ni eneo la pekee haina mipaka na majimbo mengine ya Marekani mipaka yake kwenye nchi kavu ni na Kanada (Yukon). Ncha ya Alaska inakaribia Siberia (Urusi) katika Asia kwenye mlango wa Bering.
Eneo lake ni kubwa kushinda majimbo mengine ya Marekani lakini idadi ya wakazi ni ndogo kutokana na mazingira magumu kuna wakazi 627,000 pekee (2000). Hali ya hewa ni baridi sana na katika sehemu kubwa ya jimbo hakuna uwezekano wa kulima mashamba.
Mji mkuu ni Juneau lakini mji mkubwa ni Anchorage.
Alaska iliwahi kutawaliwa na Urusi lakini iliuzwa kwa Marekani 18 Oktoba 1867. Tangu 1959 eneo lilipata hali ya jimbo la kujitawala.