Historia ya awali (kwa Kiingereza: prehistory) ni kipindi kirefu sana cha historia, kikichukua miaka yote tangu binadamu walipotokea duniani mpaka historia andishi ilipoanza (huko Mesopotamia miaka 3,300 hivi KK).[1]
Ingawa muda ni mrefu sana na ni wa msingi kwa historia yote iliyofuata, watu hawakuwa wengi kama walivyozidi kuwa kadiri ya maendeleo yao. Maisha yao hayakuwa marefu kutokana na ugumu wa mazingira na utovu wa vifaa na dawa mbalimbali.