Huntha (kwa Kiingereza: hermaphrodite, kutokana na neno la Kigiriki ἑρμαφρόδιτος, hermaphroditos) ni mmea au mnyama mwenye jinsia mbili[1].
Kwa mimea hali hiyo ndiyo ya kawaida, kumbe kwa wanyama ni 0.7%.
Inakadiriwa kuna spishi 65,000 tu kati ya 8,600,000 hivi[2] za wanyama huntha[3], lakini si binadamu, hata kama huyo amezaliwa pengine na viungo vya uzazi visivyoeleweka. Kinachotambulisha jinsia ya mtu ni chembeuzi Y kuwepo (mwanamume) au kutokuwepo (mwanamke).
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)