Saa (ala)

Saa kwenye kituo cha reli Zurich, Uswisi.
Kwa kizio cha kuhesabu mwendo wa wakati tazama saa

Saa ni kifaa kinachonyesha na kupima mwendo wa wakati. Saa ndogo huvaliwa na watu mkononi au kubebwa mfukoni, saa kubwa huwekwa ukutani au mahali pa juu mjini kwa watu wote kuona. Saa zmo ndani ya mashina na vifaa vingine vyenye kazi ya kutawala miendo yao.

Siku hizi vifaa kama simu ya mkononi hufanya kazi ya kuonyesha wakati pia.

Hii saa ya jua inaonyesha takriban saa mbili na nusu.

Watu wametazama mwendo wa wakati tangu milenia ya miaka na mwanzoni walitegemea mwendo wa jua jinsi inavyoonekana angani. Katika maeneo mbali kidogo na ikweta mwendo huu unaruhusu kutumia kuangalia mwendo wa kivuli kulingana na mwendo wa jua na hapo ni asili ya saa ya jua.

Saa ndogo ya mchanga unaonyesha dakika 5 kwa upishi wa mayai.

Mbinu mwingine ulikuwa chombo ambako ama maji au mchanga unapita kutoka chombo cha juu katika shimo ndogo kwenda chombo cha chini. Kutokana na kiwango wa ujazo wa chombo cha chini wakati hupimwa. Mifano ya kwanza ya saa ya maji inajulikana kutoka Misri. Saa ya mchanga hutumiwa hadi leo kwa mfano kwa kushika muda katika upishi.

Tangu takriban miaka 600 saa zilibuniwa zisizotegemea tena jua au maji lakini hutumia nguvu ya kamani iliyoruhusu kupunguza ukubwa na uzito na kupata saa za kubebwa na mtu mfukoni kila anapoenda.

Katika karne ya 20 mitambo ya umeme iliunganishwa na saa na seiku hizi saa nyingi huendeshwa kwa nguvu ya umeme wa beteri.

Maisha ya kisasa hutegemea saa za elektroniki na saa atomia zinazopima wakati kikamilifu hadi nanosekunde au chini yake.


Saa (ala)

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne