Tanganyika ni jina la kihistoria la sehemu kubwa ya Tanzania ya leo, yaani ile yote isiyo chini ya serikali ya Zanzibar.
Kwa sababu za kisiasa, mara nyingi huitwa "Tanzania bara" ingawa ina visiwa pia, hasa Mafia na Kilwa.
Tanganyika ilikuwa sehemu kubwa ya koloni la Ujerumani hadi vita kuu ya kwanza ya Dunia. Baada ya mwaka 1916 ilivamiwa na Uingereza na Ubelgiji. Kuanzia mwaka 1922 Tanganyika ilikuwa eneo la kudhaminiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa lililokuwa chini ya Uingereza ikawa nchi huru kati ya miaka 1961 - 1964, mwaka wa kwanza kama ufalme, halafu kama jamhuri.
Mwaka 1964 iliungana na Zanzibar na kuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.