Udhibiti wa uzazi

Udhibiti wa uzazi
Mwainisho na taarifa za nje
MeSHD003267

Udhibiti wa uzazi (pia udhibiti wa uwezo wa kuzaa au kontraseptivu) ni juhudi za kuratibu uzazi kwa sababu mbalimbali. Upangaji, utoaji na utumiaji wa udhibiti wa uzazi huitwa uzazi wa mpango.[1][2] Kwa kuacha nafasi kati ya mimba na mimba, udhibiti wa uzazi unaweza ukaboresha matokeo ya kuzaa kwa wanawake wazima na kuishi kwa watoto wao.[3] Katika ulimwengu unaokua mapato ya wanawake, rasilimali, uzito na elimu kwa watoto wao na afya huboreshwa kwa kupunguza idadi ya watoto. Udhibiti wa uzazi huweza kuongeza mapema ukuaji wa uchumi kwa sababu ya watoto wachache wanaokutegemea, wanawake wengi kushiriki katika utendakazi, na matumizi madogo ya rasilimali haba, ingawa idadi ya watoto ikipungua mno, baada ya muda wazalishaji wachache wanabebeshwa mzigo wa kutunza wazee wengi, inavyotokea katika nchi zilizoendelea.

Kwa kuwa suala hilo linahusu binadamu na uhai wake, linahitaji kukabiliwa kwa upana kuanzia maana ya utu, mwili, jinsia, upendo, uzazi n.k. Kumbe hapa zinazungumziwa tu mbinu au vifaa vinavyotumika pengine kuzuia au kuua mimba, yaani teknolojia katika ngono.[4] Jambo nyeti zaidi ni suala la mimba ya binadamu kuwa binadamu tayari, kiasi kwamba nchi nyingi zinaipatia haki fulanifulani, k.mf. ile ya kurithi. Kwa msingi huo, baadhi ya watu wanatetea uhai wa binadamu kuanzia mimba ilipotungwa na kulaumu baadhi ya vifaa vya udhibiti wa uzazi kuwa viuamimba na kusababisha vifo vya mamilioni.

  1. Oxford English Dictionary. Oxford University Press. June 2012 (online). {{cite book}}: Check date values in: |year= (help)
  2. World Health Organization (WHO). "Family planning". Health topics. World Health Organization (WHO).
  3. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named pmid22784533
  4. "Definition of Birth control". MedicineNet. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-06. Iliwekwa mnamo 9 Agosti 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Udhibiti wa uzazi

Dodaje.pl - Ogłoszenia lokalne